Nouvelle pensée : Tafuta

📍 Publié à Goma, NORD-KIVU

In stock

Hakuna kitabu kinachokuambia maisha yatakuwaje kesho.
Hakuna njia iliyoandikwa tayari kwa kila mtu.
Kila mtu ana safari yake, mapambano yake, na wakati wake.

👉 Maisha si nadharia. Ni uzoefu.

Anaye ku cheka uki tafuta, uta mu cheka utakapo pata.

Usishangae ukianza safari yako watu wakakucheka.
Wanacheka ndoto zako.
Wanacheka jitihada zako.
Wanacheka hata maumivu yako.

Lakini kumbuka:
Wale wanaocheka leo si wale watakaokucheka mwisho.

Watu hucheka kile hawakielewi.

Wanacheka kwa sababu hawajui unachokiona.
Hawajui maono yako.
Hawajui vita unavyopigana ndani yako.

Lakini siku utakapoanza kuona matokeo,
siku jitihada zako zitakapozaa matunda,
vicheko vyao vitabadilika kuwa mshangao.

👉 Wengine watanyamaza.
👉 Wengine watakupongeza.
👉 Wengine watasema “nilijua tu”.

Siri si kuwafanya wakuelewe.

Siri ni kuendelea hata usipoeleweka.
Siri ni kusimama imara hata unapochekwa.
Siri ni kuamini safari yako hata wengine wasiione.

Kwa sababu maisha hayampatii kila mtu ushindi mapema.
Lakini hayamsahau anayevumilia.

Kumbuka hili

Ukitafuta, watacheka.
Ukijitahidi, watashangaa.
Ukifanikiwa, watakupongeza.

Lakini yote haya hayapaswi kukusimamisha.

👉 Endelea.
👉 Jiamini.
👉 Songa mbele.

Achetez . Vendez . Avancez.
Maisha haina formule, lakini juhudi ya kweli haipotei kamwe. 💚

Motivation Chukudu

Motivation Chukudu

📍 Goma, NORD-KIVU 📅 Lancée il y a 8 mois
📦 20 annonces 📈 Intéressés : 16
Voir boutique
Chukudu.cd Achetez et vendez beaucoup plus facilement avec l'application
Installer l'application

Nos Catégories

⚠️CONSEILS DE SECURITE⚠️

💡 Important : En cas de problème avec un vendeur, Chukudu.cd n’est pas responsable; vous pouvez aller sur une annonce et 🚩Signaler ce vendeur, Chukudu.cd prendra des mesures.